MAUMBO NA MAANA ZA MAJINA YA ASILI YA WATU KATIKA JAMIILUGHA YA WAGOGO

MAUMBO NA MAANA ZA MAJINA YA ASILI YA WATU KATIKA JAMIILUGHA YA WAGOGO

Jemima Lenjima

27.99 €

Uchunguzi huu umechunguza maumbo na maana za majina ya asili ya watu katika jamiilugha ya Wagogo. Uchunguzi uliongozwa na nadharia ya Mofolojia Leksika kwa mujibu wa Kiparsky, (1982). Data za utafiti zilikusanywa katika mkoa wa Dodoma nchini Tanzania kwa ajili ya tasnifu ya shahada ya Uzamivu katika wilaya za Mpwapwa na Chamwino, katika vijiji vinne. Vijiji hivyo ni Mima na Gulwe kutoka katika wilaya ya Mpwapwa pamoja na vijiji vya Mvumi Misheni na Handali kutoka katika wilaya ya Chamwino vilipitiwa na mtafiti. Jumla ya watoa taarifa arobaini na nane (48) walihusika kutoa taarifa zilizohusiana na mada ya uchunguzi. Watoa taarifa hao waliteuliwa kwa kutumia usampulishaji usonasibu. Data za uchunguzi zilikusanywa uwandani kwa kutumia mbinu ya mahojiano na majadiliano ya kundi lengwa. Uchunguzi ulitumia mkabala wa kimaelezo, majedwali na baadhi ya data zilichanganuliwa kwa kutumia michorati. Matokeo ya uchunguzi yamedhihirisha kuwepo kwa makundi kumi na tatu (13) ya maumbo kwa kuzingatia aina ya jina husika na namna vijenzi vya jina hilo vilivyopangwa kupitia ngazi Leksia. Vile vile uchunguzi huu umeweza kubaini maana za baadhi ya maumbo yaliyounda nomino husika.

Pages:77
Published:2025
ISBN:979-8-89248-981-2
Language:Swahili
Category:Social & Cultural studies